1 Mimi Paulo, niliyeitwa kuwa mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na ndugu Sosthene, 2 tunawaandikia ninyi mlio kanisa la Mungu huko Korintho. Ninyi mmefanywa watakatifu katika kuungana na Kristo Yesu, mkaitwa muwe watu wa Mungu, pamoja na watu wote popote wanaomwomba Bwana wetu Yesu Kristo aliye Bwana …
1 Wakorintho 2
1 Ndugu, mimi nilipokuja kwenu sikuwahubiria siri ya ujumbe wa Mungu kwa ufasaha wa lugha, au kwa hekima ya binadamu. 2 Nilipokuwa kwenu niliamua kutojua chochote kile isipokuwa tu kumjua Yesu Kristo; naam, Kristo aliyesulubiwa. 3 Nilipokuwa kwenu nilikuwa dhaifu, natetemeka kwa hofu nyingi. 4 Hotuba zangu na mahubiri yangu …
1 Wakorintho 3
1 Ndugu, mimi sikuweza kusema nanyi kama watu mlio na huyo Roho. Nilipaswa kusema nanyi kama watu wa kidunia, kama watoto wachanga katika maisha ya Kikristo. 2 Ilinibidi kuwalisheni kwa maziwa, na si kwa chakula kigumu, kwani hamkuwa tayari kukipokea. Hata sasa hamko tayari. 3 Maana bado mu watu wa …
1 Wakorintho 4
1 Mtu na atuone sisi kuwa ni watumishi wa Kristo tuliokabidhiwa siri za mungu. 2 Kinachotakiwa kwa yeyote yule aliyekabidhiwa kazi ni kuwa mwaminifu. 3 Kwangu mimi si kitu nikihukumiwa na ninyi, au na mahakama ya kibinadamu; wala sijihukumu. 4 Dhamiri yangu hainishtaki kwa jambo lolote, lakini hiyo haionyeshi kwamba …
1 Wakorintho 5
1 Ziko habari za kuaminika kwamba kuna uzinzi miongoni mwenu; tena ni uzinzi mbaya ambao haujapata kuwako hata kati ya watu wasiomjua Mungu. Nimeambiwa eti mmoja wenu anaishi na mke wa baba yake! 2 Mnawezaje kujivuna? Ingekuwa afadhali kwenu kuomboleza, na huyo aliyefanya kitu hicho aondolewe miongoni mwenu. 3 Nami, …
1 Wakorintho 6
1 Anathubutuje mmoja wenu kumshtaki ndugu muumini mbele ya mahakama ya watu wasiomjua Mungu badala ya kumshtaki mbele ya watu wa Mungu? 2 Je, hamjui kwamba watu wa Mungu watauhukumu ulimwengu? Ikiwa basi, ulimwengu utahukumiwa nanyi, kwa nini hamstahili kuhukumu hata katika mambo madogo? 3 Je, hamjui kwamba, licha ya …
1 Wakorintho 7
1 Yahusu sasa mambo yale mliyoandika: naam, ni vizuri kama mtu haoi; 2 lakini kwa sababu ya hatari ya uzinzi, basi, kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe. 3 Mume atimize wajibu alio nao kwa mkewe, naye mke atimize wajibu alio …
1 Wakorintho 8
1 Yahusu sasa vyakula vilivyotambikiwa sanamu: Tunajua kwamba sisi sote tuna ujuzi, lakini ujuzi huo huwafanya watu wawe na majivuno; lakini mapendo hujenga. 2 Anayefikiri kwamba anajua kitu, kwa kweli hajui chochote kama inavyompasa. 3 Lakini anayempenda Mungu huyo anajulikana naye. 4 Kwa hiyo, kuhusu vyakula vilivyotambikiwa sanamu, twajua kwamba …
1 Wakorintho 9
1 Je, mimi si mtu huru? Je, mimi si mtume? Je, mimi sikumwona Yesu Bwana wetu? Je, ninyi si matokeo ya kazi yangu kwa ajili ya Bwana? 2 Hata kama kwa watu wengine mimi si mtume, lakini walau kwenu ninyi mimi ni mtume. Ninyi ni uthibitisho wa mtume wangu kwa …
1 Wakorintho 10
1 Ndugu, nataka mjue kwamba babu zetu wote walikuwa chini ya ulinzi wa lile wingu, na kwamba wote walivuka salama ile bahari. 2 Wote walibatizwa katika umoja na Mose kwa lile wingu na ile bahari. 3 Wote walikula chakula kilekile cha kiroho, 4 wakanywa pia kinywaji kilekile cha kiroho, maana …