1 Yesu aliingia tena katika sunagogi na mle ndani mlikuwa na mtu aliyekuwa na mkono uliopooza. 2 Humo baadhi ya watu walimngojea amponye mtu huyo siku ya sabato ili wapate kumshtaki. 3 Yesu akamwambia huyo mtu aliyekuwa na mkono uliopooza, “Njoo hapa katikati.” 4 Kisha, akawauliza, “Je, ni halali siku …
Luka 12
1 Wakati watu kwa maelfu walipokuwa wamekusanyika hata wakawa wanakanyagana, Yesu aliwaambia kwanza wanafunzi wake, “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani unafiki. 2 Kila kilichofunikwa kitafunuliwa, kila kilichofichika kitafichuliwa. 3 Kwa hiyo, kila mliyosema gizani, watu watayasikia katika mwanga, na kila mliyonong`ona faraghani milango imefungwa, yatatangazwa juu ya nyumba. 4 …
Marko o 4
1 Yesu alianza kufundisha tena akiwa kando ya ziwa. Umati mkubwa wa watu ulimzunguka hata ikambidi aingie katika mashua na kuketi. Watu wakawa wamekaa katika nchi kavu, kando ya ziwa. 2 Aliwafundisha mambo mengi kwa mifano, na katika mafundisho yake aliwaambia, 3 “Sikilizeni! Mpanzi alikwenda kupanda mbegu. 4 Alipokuwa akipanda, …
Luka 13
1 Wakati huo watu fulani walikuja, wakamweleza Yesu juu ya watu wa Galilaya ambao Pilato alikuwa amewaua wakati walipokuwa wanachinja wanyama wao wa tambiko. 2 Naye Yesu akawaambia, “Mnadhani Wagalilaya hao walikuwa wahalifu zaidi kuliko Wagalilaya wengine, ati kwa sababu wameteseka hivyo? 3 Nawaambieni hakika sivyo; lakini nanyi, hali kadhalika, …
Marko o 5
1 Basi, wakafika katika nchi ya Wagerase, ng`ambo ya ziwa. 2 Mara tu Yesu aliposhuka mashuani, mtu mmoja aliyepagawa na pepo mchafu alitoka makaburini, akakutana naye. 3 Mtu huyo alikuwa akiishi makaburini wala hakuna mtu aliyeweza tena kumfunga kwa minyororo. 4 Mara nyingi walimfunga kwa pingu na minyororo lakini kila …
Yohana 4
1 Mafarisayo walisikia kwamba Yesu alikuwa anabatiza na kuwapata wanafunzi wengi kuliko Yohane. 2 Lakini ukweli ni kwamba Yesu hakuwa anabatiza ila wanafunzi wake.) 3 Basi, Yesu aliposikia hayo, alitoka Yudea akarudi Galilaya; 4 na katika safari hiyo ilimbidi apitie Samaria. 5 Basi, akafika Sukari, mji mmoja wa Samaria, karibu …
Yohana 20
1 Alfajiri na mapema Jumapili, kukiwa bado na giza, Maria Magdalene alikwenda kaburini, akaliona lile jiwe limeondolewa mlangoni pa kaburi. 2 Basi, akaenda mbio hadi kwa Petro na yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, akawaambia, “Wamemwondoa Bwana kaburini, na wala hatujui walikomweka.” 3 Petro pamoja na yule mwanafunzi mwingine wakaenda …
Yohana 5
1 Baada ya hayo kulikuwa na sikukuu ya Wayahudi, naye Yesu akaenda Yerusalemu. 2 Huko Yerusalemu, karibu na mlango uitwao Mlango wa Kondoo, kulikuwa na bwawa la maji liitwalo kwa Kiebrania Bethzatha, ambalo lilikuwa na baraza tano zenye matao. 3 Humo barazani mlikuwa na wagonjwa wengi wamekaa: vipofu, viwete na …
Yohana 21
1 Baada ya hayo Yesu aliwatokea tena wanafunzi wake kando ya ziwa Tiberia. Aliwatokea hivi: 2 Simoni Petro, Thoma (aitwaye Pacha), na Nathanieli mwenyeji wa Kana Galilaya, wana wawili wa Zebedayo na wanafunzi wake wengine wawili, walikuwa wote pamoja. 3 Simoni Petro aliwaambia, “Nakwenda kuvua samaki.” Nao wakamwambia, “Nasi tutafuatana …
Yohana 6
1 Baada ya hayo, Yesu alivuka ziwa Galilaya (au Ziwa Tiberia). 2 Umati mkubwa wa watu ulimfuata kwa sababu watu hao walikuwa wameona ishara alizokuwa akifanya kwa kuwaponya wagonjwa. 3 Yesu alipanda mlimani, akaketi pamoja na wanafunzi wake. 4 Sikukuu ya Wayahudi iitwayo Pasaka ilikuwa imekaribia. 5 Basi, Yesu na …