1 Wathesalonike 1

1 Mimi Paulo, Silwano na Timotheo tunawaandikia ninyi jumuiya ya kanisa la Thesalonike, ambao ni watu wake Mungu Baba, na wa Bwana Yesu Kristo. 2 Tunamshukuru Mungu daima kwa ajili yenu ninyi nyote na kuwakumbukeni daima katika sala zetu. 3 Maana, mbele ya Mungu Baba yetu, twakumbuka jinsi mnavyoonyesha imani …

2 Wakorintho 6

1 Basi, tukiwa wafanyakazi pamoja na Mungu, tunawasihi msikubali ile neema mliyopokea kutoka kwa Mungu ipotee bure. 2 Mungu asema hivi: “Wakati wa kufaa nimekusikiliza, wakati wa wokovu nikakusaidia.” Basi, sasa ndio wakati wa kufaa, sasa ndiyo siku ya wokovu! 3 Kusudi tusiwe na lawama yoyote katika utumishi wetu, hatupendi …

1 Wathesalonike 2

1 Ndugu, ninyi wenyewe mnafahamu kwamba ziara yetu kwenu haikuwa bure. 2 Mnajua jinsi tulivyodhulumiwa na kutukanwa kule Filipi kabla ya kufika kwenu Thesalonike. Ingawa kulikuwa na upinzani mwingi, Mungu wetu alitujalia uhodari wa kuwahubirieni Habari Njema yake. 3 Jambo tunalosisitiza kwenu si jambo linalotegemea uongo au nia mbaya; wala …

2 Wakorintho 7

1 Basi, wapenzi wangu, tukiwa tumepewa ahadi hizi zote, na tujitakase na chochote kiwezacho kuchafua miili na roho zetu, tuwe watakatifu kabisa, na tuishi kwa kumcha Mungu. 2 Tunaomba mtupe nafasi mioyoni mwenu! Hatujamkosea mtu yeyote, hatujamdhuru wala kumdanganya mtu yeyote. 3 Sisemi mambo haya kwa ajili ya kumhukumu mtu; …

1 Wathesalonike 3

1 Mwishowe hatukuweza kuvumilia zaidi. Basi, tuliamua kubaki kule Athene peke yetu, 2 na kumtuma kwenu ndugu yetu Timotheo, ambaye ni mfanyakazi mwenzetu kwa ajili ya Mungu katika kuhubiri Habari Njema ya Kristo. Tulimtuma ili awaimarisheni na kuwafarijini, 3 kusudi imani ya mtu yeyote miongoni mwenu isije ikafifia kwa sababu …

2 Wakorintho 8

1 Ndugu, tunapenda kuwapa habari juu ya neema ambazo Mungu ameyajalia makanisa ya Makedonia. 2 Waumini wa huko walijaribiwa sana kwa taabu; lakini furaha yao ilikuwa kubwa hivi hata wakawa wakarimu kupita kiasi, ingawaje walikuwa maskini sana. 3 Naweza kushuhudia kwamba walikuwa wakarimu kadiri ya nguvu zao na hata zaidi. …

1 Wathesalonike 4

1 Hatimaye, ndugu zangu, mmejifunza kutoka kwetu namna mnavyopaswa kuishi ili kumpendeza Mungu. Na kweli mmekuwa mnaishi hivyo. Sasa tunawaombeni na kuwasihi kwa jina la Bwana Yesu mfanye vema zaidi. 2 Maana mnayajua yale maagizo tuliyowapeni kwa mamlaka ya Bwana Yesu. 3 Mungu anataka ninyi muwe watakatifu na mjiepushe kabisa …

2 Wakorintho 9

1 Si lazima kuandika zaidi kuhusu huduma hiyo yenu kwa ajili ya watu wa Mungu. 2 Ninajua jinsi mlivyo na moyo wa kusaidia, na nilijivuna juu yenu kuhusu jambo hilo mbele ya watu wa Makedonia. Niliwaambia: “Ndugu zetu wa Akaya wako tayari tangu mwaka jana.” Hivyo, moto wenu umekwisha wahimiza …

1 Wathesalonike 5

1 Ndugu, hakuna haja ya kuwaandikieni juu ya nyakati na majira yatakapotukia mambo haya. 2 Maana ninyi wenyewe mwajua kwamba Siku ya Bwana itakuja kama mwizi ajavyo usiku. 3 Watu watakapokuwa wanasema: “Kila kitu ni shwari na salama” ndipo uharibifu utakapowaangukia ghafla! Mambo hayo yatatukia ghafla kama uchungu wa uzazi …

2 Wakorintho 10

1 Mimi Paulo mwenyewe ambaye naonekana kuwa mpole nikiwa pamoja nanyi, lakini mkali wakati nikiwa mbali nanyi, nawasihini kwa huruma na wema wake Kristo. 2 Nawaombeni msinisababishe kuwa mkali wakati nitakapokuja, maana nina hakika naweza kuwa mkali kwa wote wale wanaotudhania kwamba tunaishi kidunia. 3 Kweli tunaishi duniani, lakini hatupigani …