1 Siku moja, watoza ushuru na wahalifu wengi walikwenda kumsikiliza Yesu. 2 Mafarisayo na walimu wa Sheria wakaanza kunung`unika: “Mtazameni mtu huyu! Anawakaribisha wenye dhambi, na tena anakula nao.” 3 Yesu akawajibu kwa mfano: 4 “Hivi, mtu akiwa na kondoo mia, akigundua kwamba mmoja wao amepotea, atafanya nini? Atawaacha wale …
Luka 16
1 Yesu aliwaambia wanafunzi wake: “Tajiri mmoja alikuwa na karani wake. Huyu karani alichongewa kwamba alitumia ovyo mali ya tajiri wake. 2 Yule tajiri akamwita akamwambia: `Ni mambo gani haya ninayosikia juu yako? Toa hesabu ya mapato na matumizi ya mali yangu, kwa maana huwezi kuwa karani tena.` 3 Yule …
Luka 17
1 Kisha, Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Haiwezekani kabisa kusitokee vikwazo vinavyosababisha dhambi; lakini ole wake mtu yule atakayevisababisha. 2 Ingekuwa afadhali kwake kufungiwa shingoni jiwe kubwa la kusagia na kutoswa baharini, kuliko kumkwaza mmoja wa wadogo hawa. 3 Jihadharini! Kama ndugu yako akikukosea, mwonye; akitubu, msamehe. 4 Na kama akikukosea …
Luka 18
1 Basi, Yesu aliwasimulia mfano kuonyesha kwamba ni lazima kusali daima bila kukata tamaa. 2 Alisema: “Katika mji mmoja kulikuwa na hakimu ambaye hakuwa anamcha Mungu wala kumjali binadamu. 3 Katika mji huohuo, kulikuwa pia na mama mmoja mjane, ambaye alimwendea huyo hakimu mara nyingi akimwomba amtetee apate haki yake …
Luka 19
1 Yesu aliingia mjini Yeriko, akawa anapita katika njia za mji huo. 2 Kulikuwa na mtu mmoja mjini, jina lake Zakayo ambaye alikuwa mkuu wa watoza ushuru tena mtu tajiri. 3 Alitaka kuona Yesu alikuwa nani, lakini kwa sababu ya umati wa watu, na kwa vile alikuwa mfupi, hakufaulu. 4 …
Luka 20
1 Siku moja, Yesu alipokuwa akiwafundisha watu Hekaluni na kuwahubiria juu ya Habari Njema, makuhani wakuu na walimu wa Sheria pamoja na wazee walifika, 2 wakasema, “Tuambie! Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani?” 3 Yesu akawaambia, “Na mimi nitawaulizeni swali: 4 mamlaka ya Yohane ya kubatiza yalitoka kwa Mungu au …
Luka 21
1 Yesu alitazama kwa makini, akawaona matajiri walivyokuwa wanatia sadaka zao katika hazina ya Hekalu, 2 akamwona pia mama mmoja mjane akitumbukiza humo sarafu mbili ndogo. 3 Basi, akasema, “Nawaambieni kweli, mama huyu mjane ametia zaidi katika hazina kuliko wote. 4 Kwa maana, wengine wote wametoa sadaka zao kutokana na …
Luka 22
1 Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa chachu, iitwayo Pasaka, ilikuwa inakaribia. 2 Makuhani wakuu na walimu wa Sheria wakawa wanatafuta njia ya kumwua Yesu, lakini waliwaogopa watu. 3 Basi, Shetani akamwingia Yuda aitwae Iskarioti, mmoja wa wale mitume kumi na wawili. 4 Yuda akaenda akajadiliana na makuhani wakuu na walinzi wa …
Luka 23
1 Kisha, wote kwa jumla, wakasimama, wakampeleka Yesu mbele ya Pilato. 2 Wakaanza kumshtaki wakisema: “Tulimkuta mtu huyu akiwapotosha watu wetu, akipinga kulipa kodi kwa Kaisari na kujiita ati yeye ni Kristo, Mfalme.” 3 Pilato akamwuliza Yesu, “Wewe ni Mfalme wa Wayahudi?” Yesu akamjibu, “Wewe umesema.” 4 Pilato akawaambia makuhani …
Luka 24
1 Jumapili, alfajiri na mapema, wale wanawake walikwenda kaburini wakichukua yale manukato waliyotayarisha. 2 Walikuta lile jiwe limeviringishwa mbali na kaburi. 3 Walipoingia ndani, hawakuona mwili wa Bwana Yesu. 4 Walipokuwa bado wanashangaa juu ya jambo hilo, mara watu wawili waliovaa mavazi yenye kung`aa sana, wakasimama karibu nao. 5 Hao …