1 Habari Njema ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.*fa* 2 Ilianza kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Tazama, namtuma mjumbe wangu akutangulie; yeye atakutayarishia njia yako. 3 Sauti ya mtu imesikika jangwani: `Mtayarishieni Bwana njia yake, nyoosheni mapito yake.”` 4 Yohane Mbatizaji alitokea jangwani, akahubiri kwamba ni lazima watu …
Marko o 2
1 Baada ya siku kadhaa, Yesu alirudi Kafarnaumu, watu wakapata habari kwamba alikuwa nyumbani. 2 Basi, wakaja watu wengi sana hata nafasi yoyote ikakosekana mlangoni. Yesu alikuwa akiwahubiria ujumbe wake, 3 wakati mtu mmoja aliyepooza alipoletwa kwake akiwa amechukuliwa na watu wanne. 4 Kwa sababu ya huo umati wa watu, …
Marko o 3
1 Yesu aliingia tena katika sunagogi na mle ndani mlikuwa na mtu aliyekuwa na mkono uliopooza. 2 Humo baadhi ya watu walimngojea amponye mtu huyo siku ya sabato ili wapate kumshtaki. 3 Yesu akamwambia huyo mtu aliyekuwa na mkono uliopooza, “Njoo hapa katikati.” 4 Kisha, akawauliza, “Je, ni halali siku …
Marko o 4
1 Yesu alianza kufundisha tena akiwa kando ya ziwa. Umati mkubwa wa watu ulimzunguka hata ikambidi aingie katika mashua na kuketi. Watu wakawa wamekaa katika nchi kavu, kando ya ziwa. 2 Aliwafundisha mambo mengi kwa mifano, na katika mafundisho yake aliwaambia, 3 “Sikilizeni! Mpanzi alikwenda kupanda mbegu. 4 Alipokuwa akipanda, …
Marko o 5
1 Basi, wakafika katika nchi ya Wagerase, ng`ambo ya ziwa. 2 Mara tu Yesu aliposhuka mashuani, mtu mmoja aliyepagawa na pepo mchafu alitoka makaburini, akakutana naye. 3 Mtu huyo alikuwa akiishi makaburini wala hakuna mtu aliyeweza tena kumfunga kwa minyororo. 4 Mara nyingi walimfunga kwa pingu na minyororo lakini kila …
Yohana 2
1 Siku ya tatu kulikuwa na arusi mjini Kana, mkoani Galilaya. Mama yake Yesu alikuwapo, 2 naye Yesu alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake. 3 Divai ilipokwisha, mama yake akamwambia, “Hawana divai!” 4 Yesu akamjibu, “Mama, usiniambie la kufanya. Saa yangu bado.” 5 Hapo mama yake akawaambia watumishi, “Lolote …
Yohana 3
1 Kulikuwa na kiongozi mmoja Myahudi, wa kikundi cha Mafarisayo, jina lake Nikodemo. 2 Siku moja alimwendea Yesu usiku, akamwambia, “Rabi, tunajua kwamba wewe ni mwalimu uliyetumwa na Mungu, maana hakuna mtu awezaye kufanya ishara unazozifanya Mungu asipokuwa pamoja naye.” 3 Yesu akamwambia, “Kweli nakwambia, mtu asipozaliwa upya hataweza kuuona …
Yohana 4
1 Mafarisayo walisikia kwamba Yesu alikuwa anabatiza na kuwapata wanafunzi wengi kuliko Yohane. 2 Lakini ukweli ni kwamba Yesu hakuwa anabatiza ila wanafunzi wake.) 3 Basi, Yesu aliposikia hayo, alitoka Yudea akarudi Galilaya; 4 na katika safari hiyo ilimbidi apitie Samaria. 5 Basi, akafika Sukari, mji mmoja wa Samaria, karibu …
Yohana 5
1 Baada ya hayo kulikuwa na sikukuu ya Wayahudi, naye Yesu akaenda Yerusalemu. 2 Huko Yerusalemu, karibu na mlango uitwao Mlango wa Kondoo, kulikuwa na bwawa la maji liitwalo kwa Kiebrania Bethzatha, ambalo lilikuwa na baraza tano zenye matao. 3 Humo barazani mlikuwa na wagonjwa wengi wamekaa: vipofu, viwete na …
Yohana 6
1 Baada ya hayo, Yesu alivuka ziwa Galilaya (au Ziwa Tiberia). 2 Umati mkubwa wa watu ulimfuata kwa sababu watu hao walikuwa wameona ishara alizokuwa akifanya kwa kuwaponya wagonjwa. 3 Yesu alipanda mlimani, akaketi pamoja na wanafunzi wake. 4 Sikukuu ya Wayahudi iitwayo Pasaka ilikuwa imekaribia. 5 Basi, Yesu na …