Mathayo 13

1 Siku hiyohiyo, Yesu alitoka katika ile nyumba, akaenda na kuketi kando ya ziwa. 2 Makundi makubwa ya watu yalimzunguka hata Yesu akapanda mashua, akaketi. Hao watu walisimama kwenye ukingo wa ziwa, 3 naye Yesu akawaambia mambo mengi kwa mifano. “Sikilizeni! Mpanzi alikwenda kupanda mbegu. 4 Alipokuwa akipanda, nyingine zilianguka …

Marko o 14

1 Ilikuwa siku mbili tu kabla ya sikukuu ya Pasaka na ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Makuhani wakuu na walimu wa Sheria walikuwa wakitafuta njia ya kumtia Yesu nguvuni kwa hila wamuue. 2 Lakini walisema, “Tusimtie nguvuni wakati wa sikukuu, watu wasije wakafanya ghasia.” 3 Yesu alikuwa Bethania, nyumbani kwa Simoni, …

Mathayo 14

1 Wakati huo, mtawala Herode alisikia sifa za Yesu. 2 Basi, akawaambia watumishi wake, “Mtu huyu ni Yohane mbatizaji, amefufuka kutoka wafu; ndiyo maana nguvu za miujiza zinafanya kazi ndani yake.” 3 Herode ndiye aliyekuwa amemtia Yohane nguvuni, akamfunga minyororo na kumtia gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, …

Marko o 15

1 Kulipopambazuka, makuhani wakuu walifanya shauri pamoja na wazee, walimu wa Sheria na Baraza lote, wakamfunga Yesu pingu, wakampeleka na kumkabidhi kwa Pilato. 2 Pilato akamwuliza Yesu, “Je, wewe ni mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Wewe umesema.” 3 Makuhani wakuu wakamshtaki Yesu mambo mengi. 4 Pilato akamwuliza tena Yesu, “Je, …

Marko o 16

1 Baada ya siku ya Sabato, Maria Magdalene, Salome na Maria mama yake Yakobo walinunua manukato ili wakaupake mwili wa Yesu. 2 Basi, alfajiri na mapema siku ya Jumapili, jua lilipoanza kuchomoza, walienda kaburini. 3 Nao wakawa wanaambiana, “Nani atakayetuondolea lile jiwe mlangoni mwa kaburi?” 4 Lakini walipotazama, waliona jiwe …

Mathayo 1

1 Yesu Kristo alikuwa mzawa wa Daudi, mzawa wa Abrahamu. Hii ndiyo orodha ya ukoo wake: 2 Abrahamu alimzaa Isaka, Isaka alimzaa Yakobo, Yakobo alimzaa Yuda na ndugu zake, 3 Yuda alimzaa Faresi na Zera (mama yao alikuwa Tamari), Faresi alimzaa Hesroni, Hesroni alimzaa Rami, 4 Rami alimzaa Aminadabu, Aminadabu …

Mathayo 2

1 Yesu alizaliwa mjini Bethlehemu, mkoani Yudea, wakati Herode alipokuwa mfalme. Punde tu baada ya kuzaliwa kwake, wataalamu wa nyota kutoka mashariki walifika Yerusalemu, 2 wakauliza, “Yuko wapi mtoto, Mfalme wa Wayahudi, aliyezaliwa? Tumeiona nyota yake ilipotokea mashariki, tukaja kumwabudu.” 3 Mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, yeye pamoja na wakazi …

Mathayo 3

1 Siku hizo Yohane Mbatizaji alitokea, akaanza kuhubiri katika jangwa la Yudea: 2 “Tubuni, maana Ufalme wa mbinguni umekaribia.” 3 Huyu Yohane ndiye yule ambaye nabii Isaya alinena juu yake aliposema: “Sauti ya mtu imesikika jangwani: `Mtayarishieni Bwana njia yake, nyoosheni vijia vyake.”` 4 Yohane alivaa vazi lililoshonwa kwa manyoya …

Mathayo 4

1 Kisha Roho alimwongoza Yesu mpaka jangwani ili ajaribiwe na Ibilisi. 2 Akafunga siku arubaini mchana na usiku, na mwishowe akaona njaa. 3 Basi, mshawishi akamjia, akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.” 4 Yesu akamjibu, “Imeandikwa katika Maandiko Matakatifu: `Binadamu hataishi kwa mikate tu, …

Mathayo 5

1 Yesu alipoyaona makundi ya watu, alipanda mlimani, akaketi. Wanafunzi wake wakamwendea, 2 naye akaanza kuwafundisha: 3 “Heri walio maskini rohoni, maana ufalme wa mbinguni ni wao. 4 Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa. 5 Heri walio wapole, maana watairithi nchi. 6 Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo …