Luka 14

1 Siku moja ya Sabato, Yesu alikwenda kula chakula nyumbani kwa mmoja wa viongozi wa Mafarisayo; watu waliokuwapo hapo wakawa wanamchunguza. 2 Mbele yake Yesu palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa na ugonjwa wa kuvimba mwili. 3 Yesu akawauliza walimu wa Sheria na Mafarisayo, “Je, ni halali au la kumponya mtu …

Luka 15

1 Siku moja, watoza ushuru na wahalifu wengi walikwenda kumsikiliza Yesu. 2 Mafarisayo na walimu wa Sheria wakaanza kunung`unika: “Mtazameni mtu huyu! Anawakaribisha wenye dhambi, na tena anakula nao.” 3 Yesu akawajibu kwa mfano: 4 “Hivi, mtu akiwa na kondoo mia, akigundua kwamba mmoja wao amepotea, atafanya nini? Atawaacha wale …

Luka 16

1 Yesu aliwaambia wanafunzi wake: “Tajiri mmoja alikuwa na karani wake. Huyu karani alichongewa kwamba alitumia ovyo mali ya tajiri wake. 2 Yule tajiri akamwita akamwambia: `Ni mambo gani haya ninayosikia juu yako? Toa hesabu ya mapato na matumizi ya mali yangu, kwa maana huwezi kuwa karani tena.` 3 Yule …

Luka 17

1 Kisha, Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Haiwezekani kabisa kusitokee vikwazo vinavyosababisha dhambi; lakini ole wake mtu yule atakayevisababisha. 2 Ingekuwa afadhali kwake kufungiwa shingoni jiwe kubwa la kusagia na kutoswa baharini, kuliko kumkwaza mmoja wa wadogo hawa. 3 Jihadharini! Kama ndugu yako akikukosea, mwonye; akitubu, msamehe. 4 Na kama akikukosea …

Luka 18

1 Basi, Yesu aliwasimulia mfano kuonyesha kwamba ni lazima kusali daima bila kukata tamaa. 2 Alisema: “Katika mji mmoja kulikuwa na hakimu ambaye hakuwa anamcha Mungu wala kumjali binadamu. 3 Katika mji huohuo, kulikuwa pia na mama mmoja mjane, ambaye alimwendea huyo hakimu mara nyingi akimwomba amtetee apate haki yake …

Luka 19

1 Yesu aliingia mjini Yeriko, akawa anapita katika njia za mji huo. 2 Kulikuwa na mtu mmoja mjini, jina lake Zakayo ambaye alikuwa mkuu wa watoza ushuru tena mtu tajiri. 3 Alitaka kuona Yesu alikuwa nani, lakini kwa sababu ya umati wa watu, na kwa vile alikuwa mfupi, hakufaulu. 4 …

Luka 20

1 Siku moja, Yesu alipokuwa akiwafundisha watu Hekaluni na kuwahubiria juu ya Habari Njema, makuhani wakuu na walimu wa Sheria pamoja na wazee walifika, 2 wakasema, “Tuambie! Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani?” 3 Yesu akawaambia, “Na mimi nitawaulizeni swali: 4 mamlaka ya Yohane ya kubatiza yalitoka kwa Mungu au …

Luka 5

1 Siku moja Yesu alikuwa amesimama kando ya ziwa Genesareti, na watu wengi walikuwa wamemzunguka wakisongana wanalisikiliza neno la Mungu. 2 Akaona mashua mbili ukingoni mwa ziwa; wavuvi wenyewe walikuwa wametoka, wanaosha nyavu zao. 3 Baada ya Yesu kuingia katika mashua moja, iliyokuwa ya Simoni, alimtaka Simoni aisogeze majini, mbali …

Luka 21

1 Yesu alitazama kwa makini, akawaona matajiri walivyokuwa wanatia sadaka zao katika hazina ya Hekalu, 2 akamwona pia mama mmoja mjane akitumbukiza humo sarafu mbili ndogo. 3 Basi, akasema, “Nawaambieni kweli, mama huyu mjane ametia zaidi katika hazina kuliko wote. 4 Kwa maana, wengine wote wametoa sadaka zao kutokana na …

Luka 6

1 Siku moja ya Sabato, Yesu alikuwa anapita katika mashamba ya ngano, na wanafunzi wake wakaanza kukwanyua masuke ya ngano, wakaondoa punje zake kwa mikono, wakala. 2 Baadhi ya Mafarisayo wakawauliza, “Mbona mnafanya jambo ambalo si halali siku ya Sabato?” 3 Yesu akawajibu, “Je, hamjasoma jinsi alivyofanya Daudi pamoja na …